Katibu mkuu wa KNUT Bwana Wilson Sossion kupitia chama hicho cha walimu,alitoa mapendekezo katika sekta ya elimu kabla shule kufunguliwa tarehe Mosi September.KNUT ilitoa hoja hizo kwa tume ya kuajiri walimu.
Baadhi ya mapendekezo makuu yaliyoangaziwa ni yafuatayo:
- Muundo wa darasani ubadilishwe.
Walimu ya shule za msingi hukadiriwa kufunza wanafunzi 50 kwa darasa ilhali wale wa sekondari ni 27.KNUT ilipendekeza TSC waajiri walimu Zaidi au wabuni mpangilio mpya ili kuleta ufanisi shuleni.
- Walimu kufunza shule kwenye maeneo wanayoishi ama kufunza shule karibu na nyumbani.Hili litaepusha kusafiri na kupunguza maambukizi na kusambaa kwa maradhi ya COVID 19.
- Tume ya kuajiri walimu itupilie mbali nafasi za walimu wa BOM na wale wa kandarasi badala yake kuwaandika kazi moja kwa moja.
- Walemavu kuzingatiwa na kupewa kipao mbele.
- Walimu wapate mafunzo ya kutosha dhidi ya mkurupuko wa maradhi ya CORONA.
Kufunguliwa kwa shule kukiwa bado ni kitendawili,Idara na Tume mbali mbali nchini bado zina wasiwasi juu ya kufunguliwa kwa shule Tarehe mosi September 2020.Ni Matumaini ya waKenya kuwa tume ya kuajiri walimu wakishirikiana na ile ya afya watayafanyia kazi mapendekezo haya.