Usahihishaji wa mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne (KCSE) 2021 utaanza Jumatatu, Waziri wa elimu Prof. George Magoha ametangaza
Akizungumza katika Shule ya Upili ya Precious Blood Riruta, Waziri alisema usahihishaji wa mtihani huo utafanyika katika vituo 35 jijini Nairobi.
“Ningependa kujulisha taifa kwamba, shughuli ya kusahihisha Mtihani wa wa KCSE 2021 tayari imeanza. Shughuli hiyo itafanyika kwa uangalifu na makini ili kuhakikisha watahiniwa wanapata alama wanazostahili,” alisema.
Mitihani ya KCSE 2021 ilikamilika Ijumaa. “Tunatumai kutoa matokeo mara tu shughuli ya usahihishaji itakapokamilika ili kuwaruhusu watahiniwa kusonga katika viwango vingine,” alisema Waziri.
Prof Magoha alisema katika kipindi chote cha wiki tatu ambapo mitihani ya KCSE 2021 ilikuwa ikifanyika, hakuna karatasi yoyote iliyovujwa kwa mtahiniwa yeyote kabla ya tarehe halisi ya mitihani hiyo.
“Vifaa vyote vya mtihani vilifikish – wa salama kwenye kontena zifaazo kabla ya kupakiwa. Vifurushi hivyo
vya mtihani havikuingiliwa kwa njia yoyote katika sehemu yoyote nchini,” alisema.
Profesa Magoha alisema ni visa vichache tu vya maafisa fisadi walio – jaribu kuingilia upakiaji wa mitihani wakiwa na lengo la kuisambaza kwa baadhi ya watahiniwa.
Alifichua kwamba, jumla ya wa – tu 50, wakiwemo mameneja wa vituo, wasimamizi, waangalizi na wafanyakazi wamekamatwa kuhusiana na jaribio la kufichua mitihani na kwamba, hatua kali itachukuliwa dhidi yao kuambatana na sheria na taratibu nyinginezo za kiusimamizi.
Jumla ya simu 300 za mkono zilipatikana kutoka kwa watahiniwa, walimu na wafanyakazi wa shule huku watu wanne waliopatikana wakijifanya watahiniwa wakati wa mtihani huo wakikamatwa.
Prof Magoha alisema watachukuliwa hatua za kinidhamu kulingana na sheria.
Awali, Magoha alifichua jinsi maafisa wa DCI walivyotibua njama ya mapema ya mtandao wa maafisa waliokuwa wakiwasaidia wanafunzi kudanganya katika mitihani yao.
- Isiolo Boys High School Hit by Fire Just Days After Nearby School Blaze
- KUPPET Suspends Teachers’ Strike Following Agreement with TSC
- Kuppet Members Under Fire: TSC Imposes Disciplinary Action
- Students Act Out Amidst Ongoing Teachers Strike
- TSC’s Standoff with KUPPET: Strike Must End Before Any Negotiation