Shule ya umma imeongoza kwa matokeo bora ya Mtihani wa Kitaifa wa Shule za Msingi (KCPE) katika kaunti ya Kwale
Shule ya Msingi ya Masimbani iliyo eneo la Lungalunga, iliongoza kaunti hiyo kwa kuzoa alama wastani ya 395.38.
Idadi kubwa ya wanafunzi waliofanya vyema katika KCPE ukanda wa Pwani walikuwa wa kutoka katika shule za kibinafsi.
Mwaka uliopita, shule hiyo ilikuwa na alama wastani ya 381.33.
Mwalimu Mkuu, Bw John Kanga, alisema matokeo hayo yalichangiwa na ushirikiano wa karibu uliopo baina ya wazazi, walimu na wanafunzi. Shule hiyo ilikuwa na watahiniwa 58 pekee.
‘Siri yetu ya ufanisi ni ushirikiano tulionao,’ akasema.
Katika orodha kamili ya matokeo ya kitaifa, Pwani haikuwakilishwa katika kumi bora.
Matokeo yaliyokusanywa kwa njia huru na Taifa Leo kufikia wakati wa gazeti hili kuchapishwa yalionyesha kuwa mwanafunzi bora Pwani alipata alama 421.
Mwanafunzi huyo ni Safari Joshua Ziro kutoka shule ya Busy Bee iliyo Kaunti ya Mombasa.
Alifuatwa na Amanya Lisa Adhiambo, kutoka Shule ya Msingi ya Amani ambayo pia iko katika Kaunti ya Mombasa.
Katika Kaunti ya Tana River, Jacob Maro Galgalo aliyeongoza kaunti kwa alama 419 alisema angelipenda kujiunga na Shule ya Upili ya Alliance kisha baadaye asomee uhandisi wa ndege.
Kwingineko Lamu, Ashraf Ali Mohamed aliyeongoza kaunti kwa alama 411 alisema matumaini yake ni kujiunga na Shule ya Upili ya Wasichana ya Alliance na kisha kusomea udaktari baadaye.
“Niliguswa sana na bidii za binamu yangu Salwa. Alipata alama 280 pekee lakini hakufa moyo. Alijiunga na shule ya wasichana ya Lamu na kujizolea alama ya B-. Baadaye akaenda Urusi kusoma. Hivi sasa amehitimu masomo ya udaktari,” akaeleza.
KCPE: Shule ya Masimbani Yaongoza Kaunti ya Kwale
- Tragic School Incident Sparks Demands for Education Leaders’ Resignation
- Isiolo Boys High School Hit by Fire Just Days After Nearby School Blaze
- KUPPET Suspends Teachers’ Strike Following Agreement with TSC
- Kuppet Members Under Fire: TSC Imposes Disciplinary Action
- Students Act Out Amidst Ongoing Teachers Strike
1 Comment
Congratulations to the Masimbani fraternity for the good work.