Site icon The Black Board Kenya

UDADISI WA INFOTRACK,CHANGA MOTO KWA SHULE KUFUNGULIWA

Udadisi mpya wa INFOTRACK uliofanywa kati ya Mwezi Mei 28 na Juni 2,wengi wa wakenya ambao ni wazazi wanaunga mkono kwa asilimia 70% shule kutofunguliwa hadi janga hili hatima yake ijulikane.Wazazi wa Pwani na Western waliongoza kwa udadisi huu kwa asilimia 77% na 64% mtawalia,wakiunga mkono shule kutofunguliwa.

Hofu kubwa ikielekezwa kwa usambaaji na maambukizi ya maradhi hayo kwa wanafunzi kwa asilimia 41% na 21% mtawalia.Hii ni kutokana na mazingira  ya shule kwa wanafunzi kuwa  wengi na kutembea makundi makundi.Mkusanyiko na mchanganyiko huu ni vigumu kudhibitiwa kwa kukosa wasimamizi wa kutosha hivyo basi kuwa changa moto kubwa kwenye maandalizi ya wanafunzi kurudi shule.Hali hii ikikadiriwa kuwa  chango kubwa kwa  maambukizi na usambaaji wa maradhi haya

Endapo mazingira  haya ya shule yatalinganishwa na nyumbani,basi nyumbani itaipiku shule kwa asilimia 58%.Wengi wa wazazi waliodadisiwa waliamini kuwa ,watoto wamelindwa na wanapata maangalizi bora majumbani.Wengi wa watoto hao wanafuata masharti ya kujikinga dhidi ya maradhi ya COVID 19.Masharti yaliotajwa yalikuwa ni kuvaa maski,kutumia viyeyuzi,kuosha mikono na kushinda nyumbani muda wote.

Udadisi huu unakuja wakati Wizara ya Afya ikishirikiana na ile ya Elimu wakijadiliana na kupanga mikakati vipi wanafunzi watarudi shule Septemba mosi.

Jee kurudi shule kutabakia kuwa ndoto?

Share the story
Exit mobile version